Kenya yapokea mabehewa 20 mapya ya abiria kutoka China ili kuongeza uwezo wa usafiri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 23, 2024

Maofisa wa Kenya wakionekana ndani ya moja kati ya mabehewa mapya ya abiria kutoka China Julai 22, 2024.

Maofisa wa Kenya wakionekana ndani ya moja kati ya mabehewa mapya ya abiria kutoka China Julai 22, 2024.

Kenya siku ya Jumatatu ilipokea mabehewa 20 mapya ya abiria kutoka China ili kuongeza uwezo wake wa usafiri na kuridhika kwa abiria wanaopanda treni.

Mabehewa hayo ni pamoja na mabehewa 10 ya daraja la pili yaliyoboreshwa, manne ya daraja la juu, moja la mgahawa, moja la nishati na manne ya daraja la kwanza.

“Maendeleo haya ni hatua muhimu kwa wizara wakati ambapo tunaendelea kuongeza ufanisi wa uendeshaji na utoaji wa huduma katika sekta ya usafiri,” Mohamed Daghar, katibu mkuu wa Wizara ya Barabara na Uchukuzi ya Kenya, amesema wakati wa hafla ya kupeperusha bendera kuashiria kupokea na kuanza kufanya kazi kwa mabehewa hayo katika mji wa pwani wa Mombasa.

Amesema kuwa kwa maendeleo hayo katika huduma za abiria, Kenya itakuwa na uwezo wa kusafirisha abiria milioni 8.8 kwa mwaka, ikijumuisha abiria milioni 6 wa safari fupi za mjini na abiria milioni 2.8 wa masafa marefu.

Mabehewa mapya ya abiria kutoka China yakifika Mombasa, mji wa bandari wa Kenya Julai 22, 2024.

Mabehewa mapya ya abiria kutoka China yakifika Mombasa, mji wa bandari wa Kenya Julai 22, 2024.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha