Wawekezaji wa EAC wapiga hatua kubwa katika kuingia kwenye soko la Kenya

(CRI Online) Julai 23, 2024

Kampuni ya kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinazidi kuongezeka na kupanua shughuli zao katika sekta muhimu za Kenya, ikiwa ni pamoja na huduma, viwanda, kilimo mafuta na gesi, na kubadili mwelekeo wa zamani ambapo kampuni za Kenya kwa muda mrefu ndizo zimekuwa zikitawala masoko ya kanda hiyo.

Wawekezaji kutoka Uganda, Tanzania, Rwanda na Somalia wamekuwa wakipanua shughuli zao nchini Kenya, na kuleta ushindani ambao haukuwepo kwa miaka mingi ambapo Kampuni za Kenya, zikiwemo benki, bima na viwanda zilikuwa zikijitanua katika soko la Afrika Mashariki kutafuta fursa mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha