Rais Kagame ashinda tena katika uchaguzi wa urais nchini Rwanda

(CRI Online) Julai 23, 2024

(Picha inatoka Xinhua)

(Picha inatoka Xinhua)

Tume ya Uchaguzi ya Rwanda imetangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa urasi jana siku ya Jumatatu, ambapo rais wa sasa wa nchi hiyo Paul Kagame ametangazwa kuwa mshindi na ataendelea na wadhifa huo.

Takwimu zilizotolewa na tume hiyo zinaonesha kuwa, Rais Kagame amepata kura zaidi ya milioni 8.8, ambazo ni sawa na asilimia 99.18 ya kura zote halali zilizopigwa na kuhesabiwa.

Mwezi Aprili mwaka 2000, Kagame aliteuliwa kuwa rais wa Rwanda katika Mkutano wa pamoja wa bunge na baraza la mawaziri, na mwezi Agosti mwaka 2003, alipata ushindi kwenye uchaguzi wa urais ulioshirikisha kwa mara ya kwanza vyama vingi vya siasa.

Kwenye uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka 2017, Kagame alipata ushindi kwa mara nyingine.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha