

Lugha Nyingine
Kenya yalenga kuwezesha vijana kwa sayansi, teknolojia ili kuchochea maendeleo
(CRI Online) Julai 24, 2024
Wizara ya Elimu ya Kenya imesema inadhamiria kutumia sayansi, teknolojia na uvumbuzi ili kuwezesha vijana na kuchochea maendeleo nchini humo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Kenya, Beatrice Inyangala kwenye kongamano la ushiriki wa wadau wa tamasha la utafiti mjini Nairobi. Amesema serikali inatoa kipaumbele kwa utafiti na ubunifu ili kutatua changamoto nyingi za kijamii.
Amesema serikali imeanzisha ushirikiano na washirika wa ndani na kimataifa ili kuendeleza ubora wa utafiti katika taasisi zote za elimu.
Ameongeza kuwa Kenya inajifunza uzoefu mzuri kutoka nchi za China, Korea Kusini, Malaysia na Singapore, ili kuchochea ukuaji wa nchi hiyo kwa njia ya kisayansi na uvumbuzi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma