

Lugha Nyingine
Afrika Kusini yalenga kuhimiza biashara kupitia jukwaa la BRICS
(CRI Online) Julai 24, 2024
Naibu waziri wa biashara, viwanda na ushindani wa Afrika Kusini Zuko Godlimpi amesema nchi yake itahudhuria mkutano wa mawaziri wa biashara wa nchi za BRICS utakaofanyika mjini Moscow, Russia, ili kutafuta fursa ya biashara na uwekezaji.
Godlimpi amesema siku ya Jumatatau, Afrika Kusini itaendelea kutafuta fursa za ushirikiano na nchi za BRICS, pamoja na ushirikiano wa pande mbili na ushirikiano kupitia jukwaa la BRICS, ambao utatoa fursa kwa bara la Afrika kuhamia kutoka nafasi yake ya kihistoria ya kuwa muuzaji malighafi na kuwa mzalishaji na muuzaji wa bidhaa zilizoongezwa thamani.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma