China yatuma salamu za rambirambi kwa Ethiopia kutokana na maafa makubwa yaliyotokana na maporomoko ya ardhi

(CRI Online) Julai 25, 2024

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema siku ya Jumatano kwenye mkutano na waadnsihi wa habari kuwa China inatuma salamu za rambirambi kwa watu walioathiriwa na maporomoko makubwa ya ardhi yaliyotokea nchini Ethiopia hivi karibuni na kusababisha hasara kubwa.

Kwa mujibu wa habari zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari, maporomoko ya ardhi yametokea hivi karibuni katika eneo la Geze Gofa, kusini mwa Ethiopia na kusababisha vifo vya watu 229, idadi ambayo huenda ikaongezeka zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha