

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China atoa wito wa kutatua mgogoro wa Ukraine kwa njia ya kisiasa
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Julai 24, 2024. (Xinhua/Lu Hanxin)
GUANGZHOU - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi siku ya Jumatano mjini Guangzhou wakati akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine aliyekuwa ziarani nchini China, Dmytro Kuleba ametoa wito wa kutatua mgogoro wa Ukraine kwa njia ya kisiasa na kuhimiza maendeleo mazuri na ya utulivu ya uhusiano kati ya China na Ukraine.
Suluhu ya kisiasa kwa mgogoro wa Ukraine
Akibainisha kuwa mgogoro wa Ukraine umeingia mwaka wake wa tatu na mgogoro huo bado unaendelea huku kukiwa na hatari ya kuongezeka na kuenea, Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema China ina nia thabiti ya kuhimiza suluhu ya kisiasa kwa mgogoro huo, na kanuni nne zilizopendekezwa na Rais Xi Jinping zinaunda msingi wa China wa kutatua mgogoro huo.
Kwa msingi huo, Wang amesema, China na Brazil kwa pamoja zimefikia makubaliano sita ya pamoja kwa ajili ya suluhu ya kisiasa kwa mgogoro huo, ikiwa ni pamoja na kanuni tatu za kudhibiti mgogoro huo, vipengele vitatu vya mpango wa amani, masuala matatu ya kibinadamu, pamoja na hatua muhimu za kuzuia hatari za nyuklia na kuhakikisha uthabiti wa minyororo ya viwanda na usambazaji.
“Makubaliano haya yamepata uungwaji mkono na mwitikio mkubwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa,” ameongeza Wang.
Kwa upande wake Kuleba amesema Ukraine inathamini sana mchango mkubwa na wa kiujenzi wa China katika kuhimiza amani na kudumisha utulivu wa kimataifa.
Upande wa Ukraine unapenda na uko tayari kufanya mazungumzo na Russia, Kuleba amesema, akiongeza kuwa majadiliano yanapaswa kuwa yenye mantiki, madhubuti na yenye lengo la kufikia amani ya haki na ya kudumu.
Maendeleo mazuri na thabiti ya uhusiano
China na Ukraine ni nchi rafiki, huku ushirikiano wao wa kimkakati ukiwa ulianzishwa muongo zaidi ya mmoja uliopita, amesema Wang, akiongeza kuwa nchi hizo mbili zinaheshimiana na kutendeana kwa usawa, na kuendeleza kwa kasi thabiti ushirikiano wa kunufaishana.
Amesema wakuu wa nchi hizo mbili wamesisitiza haja ya kuendeleza uhusiano wa pande mbili kwa mtazamo wa muda mrefu na kusukuma mbele uhusiano kati ya China na Ukraine na ushirikiano wa pande mbili.
Kuimarisha ushirikiano wenye manufaa halisi
Akibainisha kuwa mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC umeanza raundi mpya ya kuimarisha mageuzi kwa kina, Wang amesema China kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa kutaleta fursa mpya kwa watu wa nchi zote.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Julai 24, 2024. (Xinhua/Lu Hanxin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma