

Lugha Nyingine
Wataalamu wakutana nchini Kenya kujadili njia za kuboresha sekta ya maziwa barani Afrika
Watalaamu wameanza Mkutano wa Ufundi wa Sekta ya Maziwa barani Afrika mjini Nairobi, Kenya, jana Jumatano kwa lengo la kujadili njia za kuboresha sekta ya maziwa barani Afrika.
Mkutano huo ambao utafanyika kwa siku tatu unakutanisha washiriki zaidi ya 100 na ujumbe wa watu 500 unaojumuisha maofisa kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, maofisa wa ngazi ya juu wa serikali za nchi za Afrika, na wataalamu wa sekta ya maziwa, na wanabadilishana maoni kuhusu maendeleo ya kisasa ya teknolojia katika sekta hiyo ya maziwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo nchini Kenya, Jonathan Mueke amesema, nchi hiyo ilizalisha maziwa ya lita bilioni 5.2 mwaka jana, ambayo kati yake ni asilimia 40 tu yalitumika baada ya kuongezewa thamani.
Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Takwimu ya Kenya zinaonyesha kuwa, sekta ya maziwa inasaidia wakulima wadogo milioni 1.8 na kuchangia asilimia 4.5 ya uchumi wa nchi hiyo.
Kaimu mwakilishi wa FAO nchini Kenya, Tipo Nyabenyi amesema, mkutano huo utatoa jukwaa kwa sekta ya maziwa barani Afrika kutambua teknolojia za kisasa zitakazosaidia kupanua sekta ya maziwa barani humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma