

Lugha Nyingine
Rais wa Jamhuri ya Congo asema nchi yake iko tayari kushirikiana na China kuendeleza ushirikiano wenye matokeo halisi
Rais wa Jamhuri ya Congo Denis Sassou-Nguesso amesema, nchi yake iko tayari kushirikiana na China kuimarisha kuaminiana kisiasa, kuhimiza ushirikiano wenye matokeo halisi, na kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili katika kiwango cha juu zaidi.
Rais Sassou Nguesso amesema hayo alipokutana na mwakilishi maalumu wa serikali ya China kuhusu masuala ya Afrika, Bw. Liu Yuxi mapema wiki hii huko Brazzaville, mji mkuu wa nchi hiyo.
Pia amesema nchi yake inathamini urafiki wa jadi na China, na kwamba inatarajia kuhudhuria mkutano wa ujao wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika baadaye mwaka huu wa 2024, mwaka ambao pia ni wa maadhimisho ya kutimia miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Bw. Liu Yuxi amesema, China inapenda kutumia fursa ya mkutano ujao wa FOCAC, kuongezaa ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali, ili kukaribisha Maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma