

Lugha Nyingine
Tanzania yahudumia abiria milioni 3.8 waliowasili nchini humo kupitia viwanja vyake vya ndege mwaka 2023
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu ilikuwa imerekodi ongezeko la asilimia 13 la abiria waliowasili nchini humo kupitia viwanja vya ndege ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2023.
Kwenye taarifa iliyotolewa mapema wiki hii Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mussa Mbura amesema, TAA inafanya jitihada za kuboresha huduma zinazotolewa kwa watalii na wawekezaji wanaowasili nchini humo kupitia mpango wa kukarabati na kujenga vyumba vipya vya mapumziko vya abira mashuhuri (VIP) katika viwanja vya ndege vya Mwanza na Arusha, pamoja na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Amesema abiria waliowasili nchini Tanzania kupitia viwanja vya ndege wameongezeka kwa idadi ya abiria milioni 2.8 na kufikia abiria milioni 3.8 ikilinganishwa na idadi iliyorekodiwa Mwaka 2023.
Huku akisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 13, Mbura ameeleza matumaini yake kwamba majira ya baridi yatakapoanza, abiria wanaowasili nchini humo kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), KIA na Abeid Amani Karume (AAKIA) wataongezeka zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma