

Lugha Nyingine
Nigeria yalaani vitendo vya kibaguzi vya Kampuni ya Meta, ikisisitiza faini ya dola milioni 220 za kimarekani iliyoitoza
Mamlaka ya usimamizi wa ushindani ya Nigeria imesema faini ya dola milioni 220 za kimarekani iliyotozwa kampuni za teknolojia za Majukwaa ya Meta na WhatsApp za Marekani hivi karibuni imetokana na vitendo vya kibaguzi na makosa yaliyozuiwa na yenye kustahiki adhabu kisheria ambayo zimefanya.
Ikizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano mjini Abuja, Kamisheni ya Ushindani na Ulinzi wa Watumiaji Bidhaa ya Nigeria (FCCPC) imesema adhabu hiyo ya faini imetolewa kwa kampuni hizo baada ya miaka mitatu ya uchunguzi wa kina.
Kaimu Mkurugenzi wa FCCPC Adamu Abdullahi amewaambia waandishi wa habari kuwa Kampuni ya Majukwaa ya Meta imekutwa na hatia ya kunyima watu wa Nigeira data zinazohusiana na haki ya kujiamulia, uhamishaji, na utumaji wa data binafsi za watu usiodhinishwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma