

Lugha Nyingine
China na India zinapaswa kushughulikia tofauti, kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana: Wang Yi
VIENTIANE - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar mjini Vientiane, Laos siku ya Alhamisi, akisema nchi hizo mbili zinapaswa kushughulikia ipasavyo tofauti, na kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana.
Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema katika kukabiliana na hali ngumu ya kimataifa na changamoto kali za dunia nzima, China na India, zikiwa ni nchi mbili kubwa zinazoendelea na nchi mbili kubwa zenye uchumi unaoibukia ambazo zilizoko jirani, zinapaswa kuimarisha mazungumzo na mawasiliano, kuongeza maelewano na hali ya kuaminiana.
Pande hizo mbili zinapaswa kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo bora, thabiti na endelevu ya uhusiano kati ya China na India kwa moyo wa kushinda tofauti na mivutano, Wang amesema akiongeza kuwa uhusiano huo wa pande mbili una athari kubwa ambazo zinakwenda zaidi ya upeo wa pande mbili.
Uhusiano unaoboreshwa wa pande mbili unapaswa kuakisi muundo wa kimkakati wa China na India kama nchi mbili kubwa zenye kuibukia na zinazoendelea, Wang amesema.
Ameongeza kuwa, hekima ya kisiasa ya China na India zikiwa nchi mbili zenye ustaarabu wa kale inapaswa kuakisiwa katika kushughulikia tofauti zao, na umoja na ushirikiano wa nchi za Kusini unapaswa kuakisiwa katika kushughulikia changamoto za dunia nzima.
Kwa upande wake Jaishankar amesema kuwa India na China ni nchi mbili zenye watu wengi zaidi duniani, nchi mbili kubwa zenye uchumi unaoibukia na nchi mbili zenye ustaarabu wa kale wenye historia ndefu.
Amesema, kudumisha maendeleo thabiti na yenye kutabirika ya uhusiano wa pande mbili kunaendana kikamilifu na maslahi ya pande zote mbili na kuna umuhimu wa kipekee katika kulinda amani ya kikanda na kuhimiza dunia yenye ncha nyingi.
Pande hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja ili kudumisha amani katika maeneo ya mpakani na kusukuma maendeleo mapya katika mashauriano kuhusu masuala ya mpaka. Pia zimekubaliana kuimarisha mawasiliano ndani ya Jukwaa la Ushirikiano la Asia Mashariki, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, G20, BRICS na mifumokazi mingine.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma