

Lugha Nyingine
Idadi ya vifo kwenye ajali ya maporomoko ya udongo nchini Ethiopia yafikia 257
Watu wakionekana kwenye sehemu iliyotokea ajali ya maporomoko ya udongo katika eneo la Geze Gofa, kusini mwa Ethiopia, Julai 22, 2024. (Xinhua)
ADDIS ABABA - Idadi ya vifo kutokana na maporomoko ya udongo yaliyotokea Jumatatu kusini mwa Ethiopia imeongezeka hadi kufikia 257, na idadi hiyo inaweza kuongezeka hadi kufikia 500, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (UNOCHA) imesema siku ya Alhamisi.
Watu zaidi ya 15,000 walioathirika wanahitaji kuhamishwa, na serikali inapanga hatua za kuwahamisha, UNOCHA imesema katika ripoti ya hali ya mambo.
Maporomoko hayo ya udongo katika eneo la Geze Gofa kusini mwa Ethiopia yalitokea siku ya Jumatatu asubuhi wakati wa msimu wa mvua, unaokadiriwa kuendelea hadi katikati ya Septemba.
Baadhi ya watu wamefariki katika maporomoko ya ardhi yaliyofuata. Wengi bado hawajulikani waliko.
Mvua za msimu mara kwa mara husababisha maporomoko ya ardhi katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Watu wakitafuta waathirika wa ajali ya maporomoko ya udongo katika eneo la Geze Gofa, kusini mwa Ethiopia, Julai 22, 2024. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma