Idadi ya wanawake katika bunge la Rwanda yaongezeka na kufikia 63.8%

(CRI Online) Julai 26, 2024

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda imetangaza kuwa idadi ya wabunge wanawake kwenye baraza la chini la Bunge la Rwanda imeongezeka na kuwa asilimia 63.8 ya wajumbe wote 80 wa baraza hilo, ikiwa ni ongezeko la kutoka asilimia 61 kwenye bunge lililopita.

Ripoti ya mwaka 2021 iliyopewa jina la ‘Wanawake Bungeni’ iliyochapishwa na Muungano wa Mabunge ya Duniani inaonyesha kuwa Rwanda ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya wanawake katika nyadhifa serikalini. Mbali na asilimia 63.8 ya wabunge hao, nafasi 13 za uwaziri kati ya 32 zilizopo katika baraza la mawaziri la sasa zinashikiliwa na wanawake.

Miongoni mwa wabunge wanawake katika bunge jipya waliokuwepo awali, ni Christine Bakundifite aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), inayoongoza uchunguzi wa taasisi na viongozi wa serikali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha