Waziri Mkuu wa China afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Italia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 29, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Julai 28, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)

BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni siku ya Jumapili mjini Beijing, China huku pande zote mbili zikiapa kuendeleza ushirikiano wenye manufaa na faida halisi.

Akibainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Italia, Li amesema China inapenda kushirikiana na Italia ili kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, kusongesha mbele desturi ya urafiki kati ya nchi hizo mbili, kuendeleza mawasiliano na ushirikiano katika maeneo mbalimbali, kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande hizo mbili, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa amani na maendeleo ya kimataifa.

Amesema China inapenda kufanya kazi na Italia ili kuimarisha zaidi hali ya kuaminiana kisiasa, kusukuma mbele uhusiano wa pande mbili kwa mwelekeo uliokomaa na thabiti zaidi, na kuhimiza matarajio chanya ya kuzidisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Li ametoa wito kwa pande hizo mbili kuendelea kupanua biashara ya pande mbili, kuhamasisha kuboresha biashara zao, na kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja kama vile uundaji wa meli, safari za anga na za anga ya juu, nishati mpya na akili bandia, na vilevile kati ya biashara ndogo na za kati.

Kujihami kibiashara hakuwezi kulinda ushindani, na pekee ufunguaji mlango na ushirikiano ndiyo vinaweza kuleta hali ya kunufaishana na matokeo yenye manufaa kwa pande zote, Li amesema.

Kwa upande wake Meloni amesema, Italia imedhamiria kuendeleza uhusiano wa muda mrefu, thabiti na mzuri na China na inapenda kuzidisha ushirikiano wenye manufaa halisi katika uchumi, biashara, uwekezaji, viwanda, sayansi na teknolojia, utamaduni na nyanja nyinginezo.

Amesema, Italiainapenda kutoa mchango chanya katika mazungumzo ya wazi kati ya EU na China na kukuza uhusiano thabiti zaidi wa ushirikiano.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Julai 28, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Julai 28, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha