Rwanda yaweka mkazo katika mwamko wa uelewa umma kuhusu ugonjwa wa homa ya ini

(CRI Online) Julai 29, 2024

Kituo cha Matibabu cha Rwanda (RBC) kimeahidi kudhibiti maambukizi ya homa ya ini aina B na aina C nchini humo kwa kuongeza juhudi za kuongeza mwamko wa umma kuhusu uelewa wa ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa kitengo cha magonjwa ya zinaa na magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya damu katika RBC Bw. Janvier Serumondo, kwenye ujumbe wa kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani, ametoa wito kwa watu wa Rwanda kufanya upimaji wa hiari wa ugonjwa huo katika vituo vya afya vilivyo karibu yao ili kujua hali zao.

Bw. Serumondo amesema huduma za upimaji na matibabu zimegatuliwa katika vituo vya afya nchini Rwanda, ambako wanyarwanda na wakimbizi walioambukizwa nchini humo hupata huduma za matibabu bila malipo.

Pia amesema wahudumu wa afya wamepewa mafunzo, na kazi za upimaji na matibabu zimeongezeka.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha