

Lugha Nyingine
Reli ya TAZARA kusafirisha mizigo na abiria zaidi katika mwaka mpya wa fedha
Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imeidhinisha malengo ya reli hiyo kusafirisha mizigo tani laki 3.5 na abiria milioni 3.43 katika mwaka mpya wa fedha 2024/2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi mwishoni mwa wiki na makao makuu ya TAZARA, idhini hiyo imetolewa katika mkutano wa 122 wa bodi ya wakurugenzi, ambapo bodi hiyo inakadiria kupata mapato ya jumla ya dola za kimarekani milioni 55.19 katika mwaka huo mpya wa fedha ulioanza tarehe mosi Julai mwaka huu na utaisha tarehe 30 mwezi Juni mwaka 2025.
Mapato hayo yameelezwa katika ripoti hiyo kuwa yanatarajiwa kupatikana kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo usafirishaji wa mizigo, vifurushi, abiria, ada za ufikiaji huduma wazi na shughuli nyingine zisizo za uendeshaji.
Pia bodi hiyo imeeleza juhudi zinazoendelea katika kufufua reli hiyo ikishirikiana na wawekezaji kutoka China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma