

Lugha Nyingine
China na Afrika zapiga hatua kuimarisha ushirikiano wa kidijitali
Watu wakitembelea Maonyesho ya Picha kuhusu Ushirikiano wenye Matokeo halisi kati ya China na Afrika chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja jijini Nairobi, Kenya, tarehe 22 Machi 2024. (Xinhua/Han Xu)
BEIJING - Waziri wa Viwanda na Teknolojia ya Habari wa China, Jin Zhuanglong amesema kwenye Baraza la ushirikiano wa kidijitali kati ya China na Afrika siku ya Jumatatu mjini Beijing kwamba, China itafanya ushirikiano wake katika nyanja ya kidijitali na nchi za Afrika, na kuziwezesha kujenga "Afrika ya kidijitali."
Jin ameliambia baraza hilo kwamba kampuni zitaungwa mkono katika ushirikiano wa kisayansi katika maeneo kama vile mawasiliano ya simu, vituo vya data, na kebo za baharini na ardhini.
“Jitihada za pamoja pia zitafanywa kuendeleza maendeleo na matumizi ya teknolojia za kidijitali kama vile 5G, 6G, usalama wa mtandao, ufanisi wa hali ya juu wa mambo ya kompyuta na mawasiliano ya kiasi katika mifumo ya kompyuta” amesema Jin.
Pia itahamasisha kampuni, jopo la washauri bingwa na vyuo vikuu kujenga majukwaa ya ushirikiano kwa ajili ya kujenga uwezo miongoni mwa kampuni, waziri huyo ameongeza.
Mpango kazi wa maendeleo ya ushirikiano wa kidijitali kati ya China na Afrika umetolewa kwenye baraza hilo lililoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma