

Lugha Nyingine
Jumuiya ya Afrika Mashariki yatoa tahadhari kuhusu kuenea kwa homa ya nyani
(CRI Online) Julai 30, 2024
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), imetoa tahadhari kwa nchi nane wanachama na kuzitaka zitoe elimu kwa raia wao jinsi ya kujikinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa homa ya nyani (Mpox).
Tahadhari hiyo inafuatia ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba nchi mbili wanachama wa jumuiya hiyo, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), zinakabiliwa na mlipuko wa homa ya nyani.
Taarifa iliyotolewa mjini Arusha na makao makuu ya jumuiya hiyo inasema Burundi imethibitisha watu watatu kuambukizwa ugonjwa huo katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo.
WHO imesema tangu mwaka 2022, DRC imeripoti maambukizi zaidi ya 21,000 ya homa ya nyani na vifo zaidi ya 1,000.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma