

Lugha Nyingine
Kenya na Uganda katika mazungumzo ya kurefusha bomba la mafuta
Kenya na Uganda zimeanza rasmi mazungumzo ya kurefusha bomba la kusafirisha mafuta ya petroli kutoka Eldoret magharibi mwa Kenya hadi mjini Kampala.
Kampuni ya Kenya Pipeline (KPC) imesema mradi huo, unaotarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika soko la kuagiza mafuta kutoka nje ya eneo hilo, utahusisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Eldoret hadi Malaba kwenye mpaka wa Kenya na Uganda.
KPC pia imesema Uganda itakuwa na jukumu la kujenga njia ya kuunganisha bomba hilo hadi Kampala, wakati urefushaji wa baadaye utakuwa ni kuelekea mjini Kigali Rwanda.
Mkurugenzi Mkuu wa KPC Bw. Joe Sang amesema kwenye taarifa iliyotolewa mjini Nairobi kuwa, urefushaji wa bomba hilo hadi Uganda ni hatua ya kimkakati kwa Kenya wakati inatafuta kurejesha uwezo wake wa faida za kiushindani kwenye soko la kuagiza mafuta ya petrol nje ya nchi, haswa kwa kuzingatia mkakati mpya wa Uganda wa uagizaji mafuta nje ya nchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma