

Lugha Nyingine
Kenya yataka kupitia tena sera ya mambo ya nje ili kuendana na mwelekeo wa dunia
(CRI Online) Julai 31, 2024
Kenya imetoa wito wa kupitia tena sera ya mambo ya nje ya nchi hiyo ili kuendelea kuwa na umuhimu kwa nyakati za sasa na yenye ufanisi katika kuhimiza maslahi na maadili ya kitaifa.
Kiongozi wa Mawaziri wa Kenya ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje na diaspora Musalia Mudavadi amesema siku ya Jumanne kuwa, mwelekeo wa dunia unaathiri na kufafanua upya sera ya mambo ya nje ya Kenya, hivyo mwelekeo huo lazima ufikiriwe kwenye waraka wa Sera ya mambo ya nje ya Kenya ya 2024.
Ameongeza kuwa ni lazima kuendelea kutathmini na kurekebisha sera hiyo ya mambo ya nje, ili kuhakikisha inaendelea kuwa muhimu kwa nyakati za sasa na yenye ufanisi katika kuhimiza maslahi na maadili ya kitaifa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma