

Lugha Nyingine
Nchi za Pembe ya Afrika zakadiriwa kukumbwa na hali ya hewa isiyo ya kawaida
Kituo cha Utabiri na Usimamizi wa Hali ya Hewa (ICPAC) cha Mamlaka ya Kiserikali kwa ajili ya Maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD), kimetangaza Jumanne kwamba nchi za Pembe ya Afrika zinatazamiwa kukumbwa na hali ya hewa isiyo ya kawaida wiki ijayo.
Kituo hicho kimesema mvua kubwa zinazoweza kusababisha mafuriko zitanyesha katika maeneo ya kati, mashariki na magharibi mwa Sudan, kati na kusini mwa Sudan Kusini, Eritrea, kaskazini na kaskazini mashariki mwa Ethiopia, Djibouti, kaskazini mwa Uganda na magharibi mwa Kenya.
ICPAC imetoa rai kuwa watu wa jamii zilizopo katika maeneo yaliyo hatarini wanashauriwa kuwa waangalifu katika kipindi hiki.
Kwa upande mwingine, kituo hicho kimesema mvua chache kuliko kawaida zinatarajiwa katika maeneo ya mashariki na magharibi mwa Sudan Kusini, kusini-magharibi mwa Sudan, na maeneo machache katikati na magharibi mwa Ethiopia.
Mbali na utabiri huo wa kuwepo mvua kubwa, ICPAC pia imesema baadhi ya nchi za Pembe ya Afrika pia zitakuwa na joto kali ambapo nyuzi za juu kabisa zinakadiriwa kuwa zaidi ya 32 Celius.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma