

Lugha Nyingine
Afrika Kusini kupokea madishi ya SKA ya masafa ya kati kutoka China hivi karibuni
Madishi ya kwanza ya masafa ya kati ya darubini ya redio yenye eneo la Kilomita 1 ya Mraba (Square Kilometer Array-SKA), ambayo ni mtandao mkubwa zaidi wa uchunguzi wa unajimu duniani, yatasafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini, Julai 31, 2024. (Picha/People's Daily)
Madishi ya kwanza ya masafa ya kati ya darubini ya redio yenye eneo la Kilomita 1 ya Mraba (Square Kilometer Array-SKA), ambayo ni mtandao mkubwa zaidi wa uchunguzi wa unajimu duniani na mradi mkubwa wa kimataifa wa sayansi, yatasafirishwa kwenye kituo chao cha mwisho nchini Afrika Kusini kutoka China.
Kwenye hafla iliyofanyika Jumatano asubuhi kwenye eneo lililo nje kidogo ya Shijiazhuang, mji mkuu wa mkoa wa Hebei, kaskazini-magharibi mwa China, wataalam wametangaza kwamba shehena ya kwanza ya madishi manne ya masafa ya kati ya SKA, yamepita hatua ya ukaguzi wa ubora na yako tayari kusafirishwa kwa magari makubwa ya mizigo kwenda bandari ya Tianjin, ambako yatapakiwa kwenye meli hadi Afrika Kusini.
SKA ni mradi kabambe wa kisayansi unaohusisha nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na China, Uingereza na Australia. Siyo tu darubini moja ya redio, bali ni mkusanyiko wa aina mbalimbali za antena zinazoitwa safu, na zimesambazwa kwa umbali mrefu wa hadi kilomita moja ya mraba katika jumla ya eneo la kukusanya, sawa na viwanja 140 vya soka.
Mradi huo unasimamiwa na SKA Observatory, shirika la serikali mbalimbali lenye makao yake makuu mjini Manchester nchini Uingereza.
China inahusika na utafiti na uundaji wa madishi hayo ya masafa ya kati ya SKA na vile vile kutengeneza vyombo 64 vya kwanza vya namna hiyo.
Sehemu nyingi kwa ajili ya mbinuko mkubwa wa madishi, ikiwa ni pamoja na viakisi vikuu, vifaa vya servo na mkono wa usaidizi, zimesanifiwa na kuundwa na Taasisi ya 54 ya Utafiti ya Kundi la Kampuni za Teknolojia za Kielektroniki la China, iliyoko Shijiazhuang, ambayo ni mkandarasi mkuu wa China katika mradi huo wa SKA.
Yin Qiuhua, naibu meneja wa mradi huo, amesema kuwa madishi hayo manne ya kwanza yamepangwa kuwasili Afrika Kusini katika miezi ijayo na kisha kufungwa katika eneo la Karoo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma