

Lugha Nyingine
Tume ya uchaguzi ya Uganda yatangaza tarehe ya uchaguzi wa ubunge na urais wa mwaka 2026
(CRI Online) Agosti 01, 2024
Tume ya Uchaguzi ya Uganda (EC) imetoa mwongozo wa uchaguzi uliorekebishwa na kutangaza tarehe ya uchaguzi wa wabunge na rais wa mwaka 2026.
Mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi Jaji Simon Byabakama amesema kuwa uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge na urais utafanyika kuanzia tarehe 17 mwezi Septemba hadi terehe 3 mwezi Oktoba mwaka 2025.
Ameongeza kuwa kampeni zitaanza wiki ya pili ya mwezi Oktoba mwakani, na zoezi la kupiga kura litafanyika tarehe 12 Januari mwaka 2026.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma