Tume ya misaada ya Sudan yakanusha kuwepo njaa katika kambi ya IDP Kaskazini mwa Jimbo la Darfur

(CRI Online) Agosti 05, 2024

Tume ya Misaada ya Kibinadamu ya Sudan (HAC) imekanusha madai ya kuwepo njaa huko Zamzam, moja ya kambi kubwa zaidi za wakimbizi wa ndani katika Jimbo la Darfur Kaskazini magharibi mwa Sudan.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumapili, tume hiyo imesema kilichoelezwa katika ripoti ya Mtandao wa Mifumo ya Tahadhari ya Mapema ya Njaa (FEWS NET) hakina ukweli wowote.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa ripoti ya HAC katika Jimbo la Darfur Kaskazini ya Agosti 3 ilionesha kuwa ziara ya pamoja ya mashirika husika ya serikali na baadhi ya mashirika ya kimataifa kwenye kambi ya Zamzam iliyofanywa Julai 23 ilieleza hali ya utulivu wa kibinadamu huko.

Hivyo HAC imekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa uhaba wa chakula na misaada ya kibinadamu katika maeneo na kambi hizi unatokana na kuzingirwa na waasi wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) na mashambulizi ya mizinga yanayoendelea ya wanamgambo hao kwenye vituo vya afya na kambi.

Siku ya Alhamisi wiki iliyopita, FEWS NET, ilitoa tahadhari kwamba njaa inaendelea katika kambi ya Zamzam.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha