China yajenga jukwaa jipya la ujasiriamali wa China na Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 06, 2024

CHANGSHA - Ndani ya Jengo la Makao Makuu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika katika Changsha, mji mkuu wa mkoa wa Hunan, kuna sera nyingi zenye manufaa na kampuni nyingi za China na Afrika.

Kundi la Kampuni za Vymobo vya habari na Mawasiliano la China lenye makao yake makuu Taiwan, ni miongoni mwa kampuni nyingi ndani ya jengo hilo zinazotamani kupanua mtandao wake wa mauzo ya magari yanayotumia umeme barani Afrika, huku kwanza ikianzisha kampuni tanzu ndani ya jengo hilo.

"Tumetamani kwa muda mrefu kufuatilia na kuwekeza kwenye soko la Afrika, lakini safari yetu imekuwa na changamoto," anasema mwenyekiti wa kampuni hiyo Liu Yao-yuan. "Sasa kampuni nyingi zenye nia moja zinakusanyika hapa. Ninaamini mawasiliano na ushirikiano wetu unaweza kuleta ustawi wa pamoja."

Likiwa lilifunguliwa tarehe 13 Juni mwaka huu, jengo hilo ni alama mpya ya uhusiano kati ya China na Afrika huko Hunan, moja ya mikoa ya China yenye shughuli nyingi zaidi katika uhusiano wa kiuchumi na Afrika na kinara wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

Likichukua eneo lenye ukubwa wa mita za mrada zaidi ya 100,000, jengo hilo limesanifiwa kuwa makao ya kampuni za China na Afrika zinazojishughulisha na biashara na uwekezaji wa pande mbili, na kuzipatia ruzuku na huduma mbalimbali kuanzia mashauriano ya kisera hadi usaidizi wa mambo ya kifedha.

Tangu kuzinduliwa kwake, kampuni na jumuiya zaidi ya 30 katika nyanja za uhandisi, teknolojia na utafiti, mawasiliano ya simu na nyinginezo zimejikita katika jengo hilo, ambalo biashara yake na Afrika inakadiriwa kufikia thamani ya yuan bilioni 30 (dola bilioni 4.2 za Marekani) katika kipindi cha muda wa miaka mitatu ijayo.

Hafla ya uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya uchumi na biashara ya China na Afrika ikifanyika Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Juni 13, 2024. (Xinhua/Chen Zhenhai)

Hafla ya uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya uchumi na biashara ya China na Afrika ikifanyika Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Juni 13, 2024. (Xinhua/Chen Zhenhai)

Kituo cha Biashara cha Mali, ambacho ni miongoni mwa wapangaji wa kwanza wa jengo hilo, kimeanzishwa kwa lengo la kuhudumia kampuni za Mali nchini China na kusaidia kampuni za China kufanya uwekezaji katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Jumuiya ya Ushirikiano, Maendeleo na Uwekezaji ya Afrika na China yenye makao yake mjini Guangdong (ACACDI) pia inapanga kusajili kampuni katika jengo hilo, ambayo yanaahidi kusamehe kodi, kutoa ruzuku na hatua nyingine.

"Hunan ni maarufu kwa kuongoza ushirikiano wa China na Afrika," amesema Abdualla Elfrid, makamu mwenyekiti wa ACACDI. "Na tunaamini kuwa jengo hilo litakuwa daraja la kuzidisha mawasiliano, kuongeza maelewano, na kupanua ushirikiano kati ya China na Afrika."

China imeendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 15 mfululizo, huku thamani ya biashara ya pande mbili ikifikia rekodi ya dola za Marekani bilioni 282.1 Mwaka 2023, kwa mujibu wa Wizara ya Biashara ya China.

Bidhaa za ndani zikionyeshwa kwenye Jengo la Makao Makuu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Julai 22, 2024. (Xinhua/Chen Zhenhai)

Bidhaa za ndani zikionyeshwa kwenye Jengo la Makao Makuu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Julai 22, 2024. (Xinhua/Chen Zhenhai)

Baada ya kampuni binafsi nyingi zaidi kushiriki, ushirikiano kati ya China na Afrika umekuwa wa aina mbalimbali kuanzia miundombinu, madini na kilimo hadi uchukuzi, uchumi wa kidijitali, nishati safi, mambo ya fedha na mengine, amesema Xu Xiangping, mkuu wa Baraza la Kukuza Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika.

Bidhaa kutoka Afrika zikionyeshwa kwenye Jengo la Makao Makuu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Julai 22, 2024. (Xinhua/Chen Zhenhai)

Bidhaa kutoka Afrika zikionyeshwa kwenye Jengo la Makao Makuu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Julai 22, 2024. (Xinhua/Chen Zhenhai)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha