Rais wa Kenya asaini mswada mpya wa kupunguza matumizi kuwa sheria

(CRI Online) Agosti 06, 2024

Rais wa Kenya William Ruto Jumatatu alitia saini Mswada wa Matumizi ya Ziada ya Fedha kuwa sheria, unaopunguza matumizi ya serikali kwa shilingi bilioni 145.7 (kama dola bilioni 1.12 za Kimarekani).

Mswada huo mpya, ambao ulipitishwa na Bunge la Kenya Julai 31 baada ya rais kuondoa bungeni Mswada wa Fedha wa 2024 kutokana na maandamano dhidi ya serikali, unalinda matumizi muhimu, ikiwa ni pamoja na dola milioni 154 za kusaidia wakulima na kuongeza uzalishaji na tija.

Ili kuunga mkono mageuzi ya elimu, sheria hiyo mpya imetenga dola milioni 928.6, ikijumuisha uthibitishaji wa walimu wa shule, na dola milioni 238.5 kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Sheria hiyo pia imetenga dola milioni 124.6 kufadhili mageuzi ya sekta ya afya na kuhimiza Huduma ya Afya kwa Wote na dola milioni 27 kwa ajili ya nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa usalama wanaohudumu katika mashirika mbalimbali.

Juni 26, rais huyo wa Kenya aliuondoa bungeni Mswada tata wa Fedha wa 2024 ambao ulizua hasira ya umma kutokana na nyongeza nyingi za ushuru zilizochukiza watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha