Mfuko wa China wawaunga mkono watu walioko katika mazingira magumu nchini Ethiopia

(CRI Online) Agosti 06, 2024

Wizara ya Wanawake na Mambo ya Kijamii ya Ethiopia imesaini makubaliano na Mfuko wa China kwa Maendeleo ya Vijijini (CFRD), ili kutekeleza mradi wa pamoja unaolenga kuboresha maisha ya watu maskini na jamii zilizoko katika mazingira magumu kwenye maeneo mbalimbali nchini Ethiopia.

Makubaliano hayo yaliyosainiwa Jumatatu mjini Addis Ababa, yanaashiria ushirikiano na dhamira ya pande hizo mbili katika kuleta athari chanya kwa maisha ya watu wenye uhitaji.

Waziri wa Wanawake na Mambo ya Kijamii wa Ethiopia Ergogie Tesfaye amesema mfuko wa CFRD unatoa mfano mzuri katika kutoa huduma za kibinadamu nchini Ethiopia hasa katika sehemu za vijijini. Amethibitisha kuwa wizara yake inadhamiria kushirikiana na CFRD katika kutekeleza mradi huo.

Mkurugenzi wa CFRD nchini Ethiopia Yin Qian amesema mradi huo utatekelezwa mara moja baada ya makubaliano hayo kusainiwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha