

Lugha Nyingine
Kampuni za Tanzania na China zasaini mradi wa uchimbaji madini ya chuma wenye thamani ya dola milioni 77 za kimarekani
Shirika la Taifa la Maendeleo la Tanzania (NDC) na kampuni ya Hexingwang ya Fujian, China zimesaini makubaliano, ili kuendeleza mradi wa uchimbaji wa chuma wa Maganga Matitu katika mkoa wa Njombe.
Hafla ya utiaji saini wa mradi huo wenye thamani ya dola milioni 77.4 za Kimarekani utakaozalisha chuma cha sifongo kama malighafi kwa viwanda vya chuma imeshuhudiwa na Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Bw. Doto Biteko jijini Dar es Salaam.
Akitoa hotuba fupi baada ya makubaliano kusainiwa, Bw. Biteko amesema mradi huo unatarajiwa kuendeleza ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo kupitia maendeleo ya viwanda.
Mkurugenzi Mtendaji wa NDC Bw. Nicolaus Shombe amesema, mradi huo wa chuma uliopo katika eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 19.63, ni sehemu ya mradi wa chuma wa Liganga ulioko katika wilaya ya Ludewa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma