Rais Xi Jinping asisitiza kuhifadhi urithi wa kitamaduni na wa mazingira ya asili wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 07, 2024

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) katika maagizo kuhusu kuimarisha ulinzi, uhifadhi na matumizi yenye ufanisi ya mali ya urithi wa kitamaduni na wa mazingira ya asili ya China amehimiza juhudi zaidi za kuhifadhi hazina ya kitamaduni na ya mazingira ya asili ya China na kuhuisha mvuto wao katika zama mpya.

Maagizo hayo yametolewa baada ya aina moja ya mali ya urithi wa kitamaduni na aina mbili za mali ya urithi wa mazingira ya asili ya China kuingizwa kwenye Orodha ya Mali ya Urithi ya Dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mwezi Julai 2024.

UNESCO ilitangaza kuwa, Eneo la Mstari wa Katikati la Beijing: Mkusanyiko wa Majengo Yanayoonesha Mpangilio Bora wa Mji Mkuu wa China, Jangwa la Badain Jaran -- Minara ya Mchanga, Maziwa, na Hifadhi za Ndege Wanaohamahama za Pwani ya Bahari ya Manjano-Ghuba ya Bohai ya China (Awamu ya II) vimewekwa kwenye orodha yake ya mali ya urithi ya dunia kwenye mkutano mkuu wa 46 wa Kamati ya Mali ya Urithi ya Dunia ya UNESCO uliofanyika New Delhi, India.

Rais Xi amesema, kutangazwa kwa vitu hivi kuwa mali ya urithi ya dunia kuna umuhimu wa kuhimiza juhudi kwa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China ambao ni wenye umaalum wa maendeleo ya vitu na maendeleo ya maadili ya kitamaduni na mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili, yote hayo yanaongeza mng'ao mpya kwa ustaarabu wa Dunia.

Rais Xi ametoa wito wa kutumia fursa hii ya ujumuishaji huu wa UNESCO kuimarisha zaidi ulinzi wa pande zote na wenye kufuata utaratibu wa mali ya urithi wa kitamaduni na wa mazingira ya asili na kuzitumia vizuri ili kukidhi mahitaji ya watu.

Pia amehimiza kuimarishwa kwa mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa katika nyanja hii na kujitahidi kutoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia na ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Hivi sasa, China ina jumla ya Maeneo 59 ya Mali ya Urithi ya Dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha