

Lugha Nyingine
Kenya yasema mkutano ujao wa FOCAC utaimarisha uhusiano kati yake na China
Mkuu wa mawaziri wa Kenya ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora, Musalia Mudavadi amesema mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa 2024 (FOCAC) uliopangwa kufanyika Septemba mjini Beijing, utaongeza uhai katika uhusiano wa pande mbili kati ya China na Kenya ambao umedumu kwa zaidi ya miongo sita.
Akiongea kwenye mkutano na wawakilishi kutoka jumuiya za Wachina huko Nairobi, Mudavadi ameelezea matarajio ya nchi hiyo kwa mkutano huo ujao, katika uhusiano wake wa kidiplomasia na China.
Amesema ushiriki wa Kenya katika FOCAC unathibitisha azma na uungaji mkono wao usioyumba kama mshirika wa kimkakati wa China katika kuandaa mkutano wenye mafanikio.
Wawakilishi wa Ubalozi wa China nchini Kenya, Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Jumuiya ya Wachina waishio Kenya, Jumuiya ya Utalii ya Wachina nchini Kenya, Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China nchini Kenya, na kampuni za biashara za China nchini Kenya, walihudhuria mkutano huo kujadili maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ili kuhimiza pande zote mbili kunufaika.
Balozi wa China nchini Kenya Zhou Pingjian amesema uhusiano wa nchi hizo mbili umeimarika kutokana na kuaminiana na matarajio ya pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma