

Lugha Nyingine
Mafanikio kemkem ya mkutano ujao wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika yatarajiwa
Picha iliyopigwa tarehe 8, Mei, 2022 ikionesha sehemu ya Barabara ya mwendo kasi ya Nairobi, Kenya. (Picha na Xinhua)
Wachunguzi wa Afrika walisema, mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika Septemba mwaka huu unatarajiwa kupata mafanikio kemkem, na kuendeleza kwa kina uhusiano kati ya China na Afrika.
Alan Khan, msimamizi mwandamizi wa mambo ya kampuni wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Durban cha Afrika Kusini alisema, mkutano huo wa kilele utafanyika kuanzia tarehe 4 hadi 6 Septemba, na unatarajiwa kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya Afrika na China.
Benki ya Maendeleo ya Afrika ilikadiri kuwa, mahitaji ya mitaji ya kila mwaka ya ujenzi wa miundombinu ya Afrika ni kati ya dola bilioni 130 hadi bilioni 170 za kimarekani, Khan alisema mkutano huo utatoa fursa kwa kukabiliana na changamoto hii.
“China hivi sasa ni mwenzi mkubwa zaidi wa Afrika katika biashara, kwa hiyo uhusiano huo ni muhimu kwa pande zote husika, kwa kuwa pande hizo zinategemeana katika mambo ya uchumi,” alisema Khan. “Mkutano unatoa fursa kwa ushirikiano katika kuendeleza elimu, ujenzi wa miundombinu, matibabu na afya, teknolojia na sekta nyingine mbalimbali. Tunatarajia kuona ahadi na mpango wa utekelezaji kwa ajili ya kuhimiza maendeleo endelevu na ongezeko kwa pamoja.”
Khan alisema, kutokana na nchi za Afrika kufanya juhudi kubwa zaidi kuhimiza biashara ndani ya Bara la Afrika, barabara, reli na miundombinu nyingine yenye sifa bora zinahitajika ili kuunga mkono mzunguko rahisi wa bidhaa na biashara barani Afrika. Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba mkutano wa FOCAC utaupa kipaumbele ujenzi wa miundombinu, ili kuimarisha mafungamano ya mawasiliano kati ya nchi za Afrika, na mafungamano ya mawasiliano kati ya China na Afrika yalivyo kama umoja, aliongeza Khan.
Oliver Bulaya, mtetezi maalumu wa kilimo cha kisasa wa Zambia alisema, chini ya FOCAC, katika miaka 20 iliyopita, uwekezaji wa China na hatua zake za kuhimiza maendeleo zilizoongezeka zimeleta ushawishi mkubwa kwa jamii ya Zambia.
Alisema anatumai ushirikiano wa pande hizo mbili katika siku za baadaye utaweka mkazo zaidi katika kutatua changamoto kwa mazingira na jamii nchini humo, ili mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika kutoa mchango kwa ajili ya Zambia kufuata njia ya maendeleo endelevu zaidi na jumuishi zaidi.
Wakati huo huo, waziri wa kwanza wa Baraza la Mawaziri wa Kenya Musalia Mudavadi Agosti 6 alipokutana na wajumbe wa Wachina wanaoishi Kenya alisema, mkutano ujao wa Baraza la ushirikiano wa China na Afrika utaleta sura mpya kwa ushirikiano wenye matokeo halisi kati ya nchi husika na China katika sekta ya biashara na uwekezaji, ukusanyaji wa mitaji, nyumba za bei nafuu, na mawasiliano ya kiutamaduniu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma