

Lugha Nyingine
Watu 28 wauawa katika mapigano magharibi mwa Sudan
(CRI Online) Agosti 12, 2024
Watu 28 wameuawa na wengine 46 kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) katika mji wa El Fasher, mji mkuu wa mkoa wa Darfur Kaskazini magharibi mwa Sudan jumamosi iliyopita.
Kaimu Gavana wa mkoa huo, Al-Hafiz Bakheet amesema jana kuwa, wapiganaji wa kikosi cha RSF wamefanya mashambulizi katika masoko na maeneo ya raia, na kuvamia makazi ya watu na kufanya uporaji.
Kaimu Gavana huyo amesema, jeshi la Sudan na makundi yenye silaha katika kanda ya Darfur walifanikiwa kujibu mashambulio ya kikosi cha RSF na kukisababishia hasara kubwa.
Hata hivyo, kikosi cha RSF hakijatoa tamko lolote kuhusu shambulio hilo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma