Waziri Mkuu wa Libya apinga ukiukaji wa kijeshi na mafarakano nchini humo

(CRI Online) Agosti 12, 2024

Waziri Mkuu wa Libya Abdul-Hamid Dbeibah amesema serikali yake itasimama kithabiti dhidi ya mtu yoyote anayejaribu kuanzisha tena ukiukaji wa kijeshi na kuchochea mafarakano nchini humo.

Dbeibah amesema hayo wakati wa hafla ya kuhitimu kwa wanafunzi wa vyuo vya kijeshi iliyofanyika katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Amesisitiza kuwa wanaendelea kujenga jeshi lenye nguvu kwa imani ambayo msingi wake ni Mungu na taifa, na sio mtu binafsi wala kundi lolote.

Waziri Mkuu huyo amewataka wanafunzi waliohitimu kufuata nyayo za waanzilishi wa jeshi ili kuzuia matakwa ya nje na ndani ambayo yanataka kuirejesha nchi kwenye utawala wa kidikteta.

Libya imekuwa kwenye mvutano wa kisiasa tangu kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka 2011, ikiwa na serikali mbili zinazopingana na nguvu kubwa za nje zikiingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha