Idadi ya vifo kufuatia kuporomoka kwa dampo nchini Uganda yafikia 18

(CRI Online) Agosti 12, 2024

(Picha inatoka Xinhua)

(Picha inatoka Xinhua)

Idadi ya watu waliofariki kutokana na kuporomoka kwa dampo katika Wilaya ya Kawempe, Kampala, nchini Uganda, jumamosi iliyopita imeongezeka na kufikia 18.

Waziri wa Kudhibiti Maafa na Masuala ya Wakimbizi wa Uganda , Bi. Lillian Abel jana alithibitisha kuwa, miili 18 imepatikana hadi sasa, na kuongeza kuwa juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea. Aidha, serikali ya Uganda imetoa chakula na makazi ya muda kwa waathirika na inajaribu kuwahamisha kwenye maeneo ya usalama.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha