

Lugha Nyingine
Umoja wa Mataifa wasema watu 39 wameuawa nchini Somalia katika mapigano ya silaha ndani ya miezi miwili
Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema, watu 39 wameuawa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea katika miezi miwili iliyopita nchini Somalia.
Katika ripoti yake ya hali ya kibinadamu iliyotolewa jana Jumatatu mjini Mogadishu, OCHA imesema mapigano hayo yalisababishwa na mgogoro wa ardhi, ambapo watu 35 waliuawa katika Jimbo la Mudug, katikati ya Somalia, na watu wengine wanne waliuawa katika Jimbo la Luuq, kusini mwa Somalia.
OCHA pia imesema, watu 42,000, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee wamekimbia makazi yao kutokana na vurugu katika Jimbo la Luuq mwezi Julai, wakiwemo watu 12,000 waliokimbilia katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi.
Ripoti hiyo imesema, familia karibu 96,000 zimeathiriwa na mapigano ya hivi karibuni ya kutumia silaha pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi katika Jimbo la Galmudug nchini Somalia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma