Mvua kubwa na mafuriko zasababisha vifo vya watu 68 nchini Sudan

(CRI Online) Agosti 13, 2024

Waziri wa mambo ya ndani wa Sudan Bw. Khalil Pasha Sairin amesema, jumla ya watu 68 wamefariki kuanzia mwezi Juni mwaka huu kutokana na mvua kali na mafuriko yaliyozikumba sehemu nyingi nchini humo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana siku ya Jumatatu, Bw. Sairin amesema, serikali ya Sudan itatuma ujumbe wa ngazi ya juu kufanya uratibu kwenye sehemu zilizokumbwa na maafa, ambao utajumuisha maofisa kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Utabiri wa Hewa, na kutoa msaada hitajika kwa sehemu hizo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha