Africa CDC yatangaza mlipuko wa ugonjwa wa Mpox kuwa dharura ya afya ya umma barani Afrika

(CRI Online) Agosti 14, 2024

Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimetangaza ugonjwa wa Mpox kuwa janga la afya ya umma barani humo, na kuzitaka nchi za Afrika kuchukua hatua za haraka ili kuzuia ugonjwa huo kuendelea kuenea katika bara hilo.

Mkurugenzi wa Africa CDC Bw. Jean Kaseya amesema jana Jumanne kuwa, uamuzi huo utasaidia kukusanya rasilimali kwa kiasi kikubwa, kuimarisha utaratibu wa kimataifa wa kutoa taarifa, na kukabiliana vyema na janga hilo.

Takwimu za Alhamis wiki iliyopita kutoka kituo hicho zilionyesha kuwa nchi 16 barani Afrika zimeathiriwa na ugonjwa wa Mpox.

Afrika imeripoti ongezeko la asilimia 160 la maambukizi ya Mpox mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha