Wadau kutoka China na Afrika wakutana nchini Kenya na kutoa wito wa kufanya mageuzi katika mfumo wa chakula

(CRI Online) Agosti 14, 2024

Mkutano na waandishi wa habari ukifanyika wakati wa Jukwaa la Sayansi la Afrika-China-CIMMYT mjini Nairobi, Kenya, Agosti 13, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Mkutano na waandishi wa habari ukifanyika wakati wa Jukwaa la Sayansi la Afrika-China-CIMMYT mjini Nairobi, Kenya, Agosti 13, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Watunga sera, wanasayansi na wamiliki wa viwanda kutoka China, Afrika, na Kituo cha Kimataifa cha Uboreshaji wa Mahindi na Ngano (CIMMYT) wamekutana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, na kuzindua jukwaa linalolenga kuendeleza mageuzi ya kilimo, kufikia usalama wa chakula, na kukabiliana na umasikini katika maeneo ya vijijini barani Afrika.

Jukwaa la Kisayansi la Kituo cha Kimataifa cha Uboreshaji wa Mahindi na Ngano la China na Afrika, lililoandaliwa na Akademia ya Sayansi ya Kilimo ya China (CAAS) pamoja na Kituo hicho, limejikita katika Kubadili Mifumo ya Kilimo barani Afrika kupitia Uvumbuzi wa Kisayansi na Uhusiano.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo hicho Bram Govaerts amesisitiza umuhimu wa jukwaa hilo, akisema linatoa fursa muhimu kwa wanasayansi wa China na Afrika kutafiti mikakati mipya ya kubadili mifumo ya chakula huku kukiwa na changamoto kama vile mabadiliko ya tabianchi, wadudu waharibifu wa mimea na magonjwa.

Makamu Mkuu wa CAAS Ye Yujiang amesema, uhusiano wa kunufaishana kati ya wanasayansi wa China na Afrika unaweza kuchochea mageuzi ya kilimo, kuboresha usalama wa chakula na lishe, na kuboresha kipato cha vijijini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha