

Lugha Nyingine
Kampuni ya China yawekeza katika ujenzi wa kituo kikubwa zaidi cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua nchini Botswana
Kampuni ya Umeme ya Botswana imesaini mkataba wa ununuzi wa umeme na Kampuni ya Sinotswana Green Energy, na kuanza rasmi ujenzi wa kituo cha kwanza cha kuzalisha umeme wa nishati ya jua chenye uwezo wa megawati 100 nchini Botswana.
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi amesema huu ni mradi muhimu wa Botswana unaoendana na malengo ya sera za nishati ya nchi hiyo ambayo yanaweza kuzalisha nishati himilivu, ya kuaminika na ya kutosha kwa maendeleo endelevu.
Konsuli wa mambo ya uchumi katika Ubalozi wa China nchini Botswana Lan yuqiang amesema, China iko tayari kubadilishana uzoefu wa kuendeleza nishati ya kijani na Botswana, na kuhamasisha kampuni nyingi zaidi za China kuwekeza katika sekta ya nishati mpya nchini Botswana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma