China na Afrika zakumbatia uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kibiashara

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 15, 2024

Muonyeshaji akionyesha bidhaa za kahawa kwenye Maonyesho ya Kiuchumi na Kibiashara ya China na Afrika barani Afrika (Kenya) 2024 jijini Nairobi, Kenya, Mei 9, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Muonyeshaji akionyesha bidhaa za kahawa kwenye Maonyesho ya Kiuchumi na Kibiashara ya China na Afrika barani Afrika (Kenya) 2024 jijini Nairobi, Kenya, Mei 9, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

BEIJING - China na nchi za Afrika zimeendeleza uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kibiashara huku kukiwa na kuongezeka kwa thamani ya biashara, na anuai ya bidhaa na huduma kutoka pande zote mbili, takwimu zilizotolewa hivi karibuni zimeonyesha.

Thamani ya biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kwa asilimia 5.5 mwaka hadi mwaka kufikia yuan trilioni 1.19 (dola karibu bilioni 166.6 za Kimarekani) kati ya Januari-Julai, takwimu kutoka kwa Idara Kuu ya Forodha ya China (GAC) zinaonyesha.

China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 15 mfululizo, takwimu hizo za forodha zimeonyesha.

Thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia rekodi ya juu ya dola za Marekani bilioni 282.1 Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.5 mwaka hadi mwaka, ikionyesha uhimilivu mkubwa.

Mwaka 2023, mauzo ya nje ya China ya magari yanayotumia nishati mpya, betri za lithiamu, na bidhaa za kuzalisha umeme kwa nishati ya jua barani Afrika yaliongezeka kwa asilimia 291, asilimia 109 na asilimia 57 mwaka hadi mwaka, mtawalia.

Wakati huo huo, uagizaji wa China wa karanga, mboga, maua na matunda kutoka Afrika uliongezeka kwa asilimia 130, asilimia 32, 14 na asilimia 7, mtawalia, ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Hasa, biashara kati ya China na Afrika katika bidhaa za kuzalisha bidhaa nyingine iliongezeka kwa asilimia 6.4 mwaka hadi mwaka katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, takwimu hizo za GAC ​​pia zinaonyesha.

Biashara ya bidhaa za kuzalisha bidhaa nyingine kati ya China na Afrika inachukua asilimia 68 ya thamani ya jumla ya biashara kati ya pande hizo mbili, ikiisaidia Afrika katika mchakato wake wa maendeleo ya viwanda na juhudi za kuufanya uchumi wake uwe wa aina mbalimbali, amesema Lyu Daliang, afisa wa GAC.

Sang Baichuan, Mkuu wa Taasisi ya Uchumi wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Biashara na Uchumi wa Kimataifa, amesema biashara kati ya China na Afrika imekua kwa kasi kutokana na ushirikiano wa kunufaishana.

Mkutano wa Kilele wa Mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika Beijing kuanzia Septemba 4 hadi 6, na unatarajiwa kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili, Lyu amesema.

Kaulimbiu ya mkutano wa FOCAC wa Mwaka 2024 ni "Kushikana Mikono Kuhimiza Ujenzi wa Mambo ya Kisasa na Kujenga Jumuiya ya Ngazi ya Juu ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja," tangazo lililotolewa na wizara ya mambo ya nje ya China Julai 30 linasema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha