

Lugha Nyingine
China yaitaka jamii ya kimataifa kuheshimu uhuru na uongozi wa Sudan Kusini katika kipindi cha mpito wa kisiasa
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kuheshimu uhuru na uongozi wa Sudan Kusini katika kipindi cha mpito wa kisiasa, na kuepuka kuiwekea shinikizo au taratibu kutoka nje.
Balozi Dai amesema hayo katika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Sudan Kusini.
Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuiunga mkono Sudan Kusini katika kutekeleza Mkataba Uliohuishwa wa Amani, kuhimiza pande zote kushiriki katika mazungumzo ya kisiasa, kuimarisha mshikamano na kuaminiana, na kutafuta makubaliano mapana zaidi ya kisiasa kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Amesisitiza kuwa Sudan Kusini ina hali yake ya kipekee, na watu wa nchi hiyo wana haki ya kujiamulia hatma ya nchi yao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma