Kuongezeka kwa joto la baharini kwaleta changamoto kwa wakulima wanawake wa mwani Zanzibar

(CRI Online) Agosti 15, 2024

Wakati kilimo cha mwani kimekuwa shughuli kubwa ya kiuchumi kwa maelfu ya wanawake katika Visiwa vya Zanzibar, nchini Tanzania, kuongezeka kwa joto la maji ya bahari kumeanza kuleta changamoto kwenye maisha ya kila siku ya wakulima hao.

Kilimo cha mwani kimekuwa ni biashara yenye faida kwa wanawake hao, lakini mavuno kidogo kutokana na kuongezeka kwa joto la bahari kunaleta ugumu kwa wanawake hao kujikimu kimaisha.

Baadhi ya wanawake walianza kuzoea kuvuna madodoki ya baharini. Madodoki hayo hustahimili joto na huchuja maji taka na kemikali kwenye maji.

Wanaharakati wa haki za wanawake wa Zanzibar wanaona kilimo hicho kinasaidia kuboresha usawa wa kijinsia visiwani Zanzibar na kinaondoa wanawake hao kutoka kwenye umaskini.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha