

Lugha Nyingine
Wanafunzi zaidi ya 300 wa Ethiopia wapata ufadhili wa masomo unaotolewa na serikali ya China
Wanafunzi zaidi ya 300 wa vyuo vikuu nchini Ethiopia wamepata ufadhili wa masomo unaotolewa na serikali ya China ili kuwawezesha kuendelea na masomo ya juu katika nyanja mbalimbali za elimu katika vyuo vikuu vya nchini China.
Hafla maalum ya kuwaaga wanafunzi hao imefanyika jana Alhamisi katika Ubalozi wa China nchini Ethiopia na kuhudhuriwa na maofisa wa serikali ya Ethiopia, wanadiplomasia wa China nchini Ethiopia, na familia za wanafunzi waliopata ufadhili huo.
Mkuu wa Dawati la Ufadhili wa Masomo wa Kimataifa katika Wizara ya Elimu nchini Ethiopia Idossa Terfasaa amesisitiza umuhimu wa ongezeko la ufadhili unaotolewa na China kama sehemu ya uhusiano mpana wa nchi hizo mbili katika ujenzi wa uwezo.
Konsuli mkuu katika Ubalozi wa China nchini Ethiopia Shen Qinmin ametoa wito kwa wanafunzi hao wa Ethiopia kufanya vizuri katika masomo yao na kutoa mchango wenye matokeo halisi kwa maendeleo ya baadaye ya nchi yao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma