Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China: Nchi nyingine zinakaribishwa kuongeza uwekezaji barani Afrika kama China inavyofanya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 29, 2024

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian tarehe 28 alisema kuwa, kuunga mkono maendeleo ya Afrika ni jukumu la pamoja la jumuiya ya kimataifa. China inakaribisha nchi nyingine kutilia maanani kuongeza uwekezaji wao kwa Afrika kama inavyofanya China, na China ingependa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kuhimiza kwa pamoja maendeleo na ustawi wa Afrika na kuleta manufaa kwa watu wa Afrika.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari wa siku hiyo, mwandishi wa habari aliuliza kuwa, hivi karibuni aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa UNDP nchini Kenya, ambaye pia ni mtaalamu wa uchumi wa Kenya Hannah Ryder alipohojiwa alisema, kwa kushirikiana na China, nchi za Afrika hazina haja ya kulazimika kubadilisha sera zao zenyewe. Kufanya ushirikiano kutokana na mahitaji ya Afrika ni sifa wazi ya ushirikiano kati ya Afrika na China, hali hii pia imezifanya nchi za Magharibi na washirika wengine wengi wa ng’ambo kuzingatia zaidi mahitaji ya Afrika na kuanzisha uhusiano wa wenzi wenye usawa na Afrika. Jarida la Marekani “The National Interest” lilichapisha makala likisema kuwa, China inatoa bidhaa nyingi za kiumma kwa nchi zinazoendelea, zikiwemo zile za Afrika, na inashinda ushawishi wake katika "Kusini ya Dunia." Je, msemaji una maoni gani kuhusu hayo?

Lin Jian alisema kuwa siku zote China inashikilia dhana ya ukweli, uhalisia, urafiki na udhati na mtazamo sahihi wa haki na faida katika ushirikiano kati yake na Afrika, na maslahi ya kimsingi ya watu wa China na Afrika ni lengo la tangu mwanzo hadi mwisho.

Alisema kuunga mkono maendeleo ya Afrika ni jukumu la pamoja la jumuiya ya kimataifa. Ikiwa nchi moja ya "Kusini ya Dunia," China haitafuti "kushinda ushawishi katika 'Kusini ya Dunia,'" bali inajikita katika kuunga mkono wenzi wake wa "Kusini ya Dunia," wakiwemo wa Afrika, kufikia maendeleo na ustawi wa kweli. China pia haishiriki kwenye ushindani wa kisiasa wa kijiografia barani Afrika, bali inafurahia kuona nchi zote zikitoa mchango wa kivitendo kwa maendeleo ya Afrika.

"Tunakaribisha nchi nyingine kuzingatia zaidi kuongeza uwekezaji wao kwa Afrika kama inavyofanya China, na kuwa na kuutendea kwa dhana ya uwazi uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika. Pia tungependa kufanya ushirikiano wa pande tatu au pande nyingi kwenye msingi wa kuheshimu matakwa ya upande wa Afrika," alisema Lin Jian.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha