Matokeo mengi mapya ya teknolojia yaonyeshwa kwenye Maonesho ya Viwanda vya Data Kubwa 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2024

Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda vya Data Kubwa 2024 yalifunguliwa tarehe 28, Agosti. Picha na Yang Qian/People’s Daily Online

Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda vya Data Kubwa 2024 yalifunguliwa tarehe 28, Agosti. Picha na Yang Qian/People’s Daily Online

Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda vya Data Kubwa ya China 2024 yalifunguliwa kwenye mji wa Guiyang, Mkoa wa Guizhou Tarehe 28, Agosti.

Maonyesho hayo yameshirikishwa na kampuni na mashirika 414 kutoka ndani na nje ya China, yakionesha teknolojia mpya za kidijitali, masuluhisho na matumizi yenye uvumbuzi wa viwanda hivyo.

Habari zinasema kuwa maonyesho hayo yana kauli mbiu ya “Kuishi pamoja kwa data kubwa na teknolojia za kisasa: Kujenga mustakabali mpya wa uchumi wa kidijitali yenye maendeleo ya kiwango cha juu”, na yamepanga eneo la maonesho lenye ukubwa wa kilomita za mraba 60,000.

Katika Maonesho hayo, shughuli mbalimbali, zikiwemo mawasiliano kati ya wadau wa viwanda husika, shughuli za kutangaza matokeo mapya, mashindano ya “mambo ya data” zitafanyika, ili kuonesha kwa pande zote maendeleo mapya ya viwanda vya dijitali ndani na nje ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha