Lugha Nyingine
Mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Mambo ya Amerika Kaskazini na Oceania ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China atoa habari kuhusu ziara ya Jake Sullivan nchini China
Usiku wa tarehe 29, Agosti, mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Mambo ya Amerika Kaskazini na Oceania ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China Yang Tao alitoa habari kwa vyombo vya habari kuhusu ziara ya msaidizi wa rais wa Marekani wa mambo ya usalama wa nchi Bw. Jake Sullivan nchini China.
Yang alisema, kutokana na mwaliko wa Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati kuu ya Chama, Bw. Jake Sullivan alifanya ziara nchini China kuanzia tarehe 27 hadi 29 Agosti kwa kufanya mazungumzo ya duru mpya ya kimkakati kati ya China na Marekani. Hii ni ziara ya pili nchini China kwa ofisa wa cheo hicho wa Marekani baada ya miaka minane iliyopita.
Yang alisema, rais Xi Jinping alikutana na msaidizi Sullivan mchana wa tarehe 29, Agosti. Rais Xi alisisitiza kuwa, kwanza, kwa mawasiliano kati ya China na Marekani, mambo muhimu ni kuwa na utambuzi sahihi wa kimkakati, ni kwanza lazima kujibu vizuri kuhusu China na Marekani ni wapinzani au ni wenzi, hili ni suala linalohusiana na mambo ya jumla. China inashikilia kufuata njia ya kujiendeleza kwa amani, inapotimiza maendeleo yake yenyewe, ingependa pia kutafuta maendeleo kwa pamoja na nchi nyingine na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Pili, kwa kukabiliwa na hali ya kimataifa yenye mabadiliko yanayochanganikiwa na fujo, nchi mbalimbali zinahitaji mshikamano na ushirikiano badala ya mafarakano na mapambano. China na Marekani zikiwa nchi kubwa zinatakiwa kuwa chanzo cha utulivu kwa amani ya dunia na msukumo wa maendeleo ya pamoja.
Tatu, upande wa China haujabadilisha lengo lake la kujikita katika kuufanya uhusiano kati ya China na Marekani uendelezwe vizuri kwa utulivu, na kupata maendeleo endelevu. Anatumai upande wa Marekani utakuwa na mantiki ya kuleta hamasa kwa kuitendea China na maendeleo ya China, na kuchukulia maendeleo ya kila upande ni fursa kwa upande mwingine bali si changamoto.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma