Ushirikiano kati ya China na Afrika wahimiza mageuzi ya nishati barani Afrika

(CRI Online) Agosti 30, 2024

Kutokana na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, China na nchi za Afrika zimekuza kwa ushirikiano mageuzi ya nishati barani Afrika.

Hayo yamesemwa na Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Kamati hiyo imesema, China na Afrika zimehimiza kikamilifu ushirikiano wa kiutendaji katika kuendeleza nishati safi, kuunga mkono makampuni ya China kuanzisha miradi ya nishati inayotumia teknolojia za kisasa na kutoleta uchafuzi kwa mazingira katika nchi na sehemu zaidi ya 40 barani Afrika, ikihusisha sekta za nishati ya photovoltaic, uzalishaji wa umeme kwa nishati ya upepo na maji, na biomass.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mambo ya Kimataifa katika Mamlaka ya Nishati ya China Dong Xiang ameeleza kuwa, ushirikiano kati ya China na Afrika umehimiza makampuni ya China kushiriki katika ushirikiano wa nishati barani Afrika, ili kuboresha maisha ya watu wa huko na kuhimiza maendeleo ya kijani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha