Lugha Nyingine
Rais Xi akutana na mwenzake wa DRC
(Picha na Yin Bogu/Xinhua)
Rais Xi Jinping wa China alikutana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi Jumatatu hapa Beijing.
Tshisekedi yupo Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Akikumbuka kuwa China na DRC ziliinua uhusiano wa nchi hizo mbili hadi kufikia ushirikiano wa kimkakati mwezi Mei 2023, Rais Xi amesema pande hizo mbili zimekuwa zikiendeleza ushirikiano wa kivitendo katika sekta mbalimbali tangu kuboreshwa kwa uhusiano baina ya nchi hizo mbili na kuwa mfano wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea kukuza juhudi za pamoja za kuelekea kuwa nchi za mambo ya kisasa.
Alisema China inapenda kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa na kutafuta maendeleo kwa pamoja na DRC, kuzidisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika kilimo, uchakataji wa madini na mafunzo ya kazi za ufundi stadi, na kuendelea kuisaidia DRC kubadilisha tija ya rasilimali kuwa chachu ya ukuaji.
Rais Xi amesisitiza kuwa katika mkutano ujao wa kilele wa FOCAC, China na Afrika zitatangaza msimamo mpya wa uhusiano kati ya China na Afrika na mfululizo wa hatua muhimu za kuendeleza kwa pamoja mambo ya kisasa na hivyo kuweka muongozo mpya wa uhusiano kati ya China na Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma