

Lugha Nyingine
China yaadhimisha miaka 79 tangu ushindi wa vita dhidi ya uvamizi wa Japan na vita dhidi ya ufashisti duniani
Shi Taifeng, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Muungano ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akihudhuria kongamano la kuadhimisha miaka 79 tangu ushindi wa Vita vya Watu wa China Dhidi ya Uvamizi wa Japan na vita vya kimataifa dhidi ya ufashisti, mjini Beijing, China, Septemba 3, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)
BEIJING - Kongamano limefanyika siku ya Jumanne mjini Beijing kuadhimisha miaka 79 tangu ushindi wa Vita vya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan na vita vya kimataifa dhidi ya ufashisti.
Shi Taifeng, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Muungano ya Kamati Kuu ya CPC, alihudhuria kongamano hilo.
Shi amesema kuwa ushindi mkubwa katika Vita dhidi ya Uvamizi wa Japan ulilinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China, uliashiria ushindi kamili katika vita vya kimataifa dhidi ya ufashisti, kuthibitisha tena China kuwa nchi kubwa duniani, na kuletea watu wa China heshima kwa watu wote wapenda amani duniani kote.
Viongozi wa Idara ya Muungano wa Kamati Kuu ya CPC, Taasisi ya Historia ya Chama na Maandishi ya Kamati Kuu ya CPC na Idara ya Kazi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, askari wastaafu na wanafunzi vijana walizungumza kwenye kongamano hilo.
Walikumbuka jinsi watu wa China walivyopigana vita hivyo, walichangia uelewa wao juu ya umuhimu wa ushindi huo, na wameelezea dhamira yao kwa amani na maendeleo.
Watu takriban 200 walishiriki kwenye kongamano hilo, wakiwemo jamaa za wanajeshi na maofisa wastaafu, na mashujaa waliopigana kwenye vita hivyo, pamoja na raia wa kigeni waliotoa uungaji mkono kwa watu wa China katika vita hivyo au jamaa zao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma